News
Zoezi la Urasimishaji Ardhi Zanzibar Lashika Kasi
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, hivi karibuni imeanza zoezi la urasimishaji ardhi katika maeneo 15 ya Unguja. Zoezi hili limeanza na hatua ya utambuzi lengo likiwa ni kuyatambua maeneo hayo na kuwapatia wananchi hati ya haki ya matumizi ya ardhi. Maeneo yanayohusika na zoezi hili ni pamoja na Shakani, Uroa, Mombasa, Meya Kidoti, Fuoni, Gombani, Amani, Mahonda, Konde, Utaani, Pemba ni Bopwe, Kwamchina, Micheweni na Jambiani.
Aidha shughuli ya urasimishaji katika maeneo ya Shehia hizi imehusisha uhamasishaji na utoaji wa elimu kwa wananchi. Uhamasishaji na utoaji elimu pia umefanyika ambapo elimu imetolewa kwa Wakuu wa mikoa na Wilaya na waliahidi kuwa watahakikisha elimu hiyo wanaipeleka kwa watendaji pamoja na wananchi wenyewe hadi kukamilika kwa zoezi zima la urasimishaji katika meneo hayo 15.