Tanzania emblem

The United Republic of Tanzania

Property and Business Formalization Program

News

UTOAJI WA HATI WILAYA YA MAKETE


Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) imekabidhi zaidi ya hatimiliki za ardhi 135 kwa wakazi wa Tandala na Ikonda wilayani Makete. Hafla hiyo ya kukabidhi hati hizo imefanyika eneo la Tandala, Kata ya Ikonda wilayani Makete, Septemba 24, 2022, ikihudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MKURABITA, Dkt. Seraphia Mugembe, Mbunge wa jimbo hilo, Festo Sanga, Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya, Alex Ngailo ambaye alikuwa mgeni rasmi pamoja na viongozi wengine mbalimbali.