Tanzania emblem

The United Republic of Tanzania

Property and Business Formalization Program

News

Wasomi kutoka Chuo Kikuu Ardhi watinga MKURABITA Makao Makuu Dodoma


Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu Ardhi, Skuli ya Mipango Miji na Sayansi ya Jamii leo tarehe 19 Mei 202 wametembelea Ofisi MKURABITA zilizopo Dodoma kwa lengo la kujifunza shughuli zinazofanywa na Mpango huu. Aidha wanafunzi hao wa ngazi ya Uzamili wanatarajia kutembelea baadhi ya Halmashauri zilizojengewa uwezo na MKURABITA katika utekelezaji wa kazi za urasimishaji ardhi na biashara. Halmashauri hizi ni pamoja na Chamwino, Mpwapwa kujione hali ya uendelevu wa urasimishaji ardhi. Pia wanatarajia kutembelea Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam – Ilala ambako kimejengwa Kituo Jumuishi cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara kwa ushirikiano baina ya MKURABITA na Halmashauri hiyo.