Tanzania emblem

The United Republic of Tanzania

Property and Business Formalization Program

News

Wananchi wa Nangara Ziwani, Babati waahidi kuwa mabalozi wa Urasimishaji Ardhi


Wananchi 120 waliorasimishiwa viwanja vyao katika Mtaa wa Nangara Ziwani Kata ya Nangara Ziwani Halmashauri ya Mji Babati walikabidhiwa hati miliki na Mgeni Rasmi Ndugu Mathias Mkumbo akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Babati. Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Ndg. Mkumbo alishukuru MKURABITA kwa kuwezesha zoezi la urasimishaji wa viwanja 1,000 ambapo hadi sasa viwanja 500 vimerasimishwa. Pia aliwashukuru wananchi kwa wa Babati kwa utayari wao na kuitikia zoezi hilo la urasimishaji. Hata hivyo aliwasihi wale waliopata hati kwenda kuwa mabalozi wazuri kwa wananchi wengine.

Kwa upande wa MKURABITA, Bw. Mwesiga Ileta ambaye alimwakilisha Mratibu wa Mpango, aliushukuru Uongozi wa Halmashauri kwa ushirikiano ambao umefanikisha utekelezaji wa zoezi hilo. Aidha, aliwasihi wana Babati kuhakikisha mchakato huo unakuwa endelevu ili kuweza kuwafikia wanachi walio wengi.

Nao wananchi walionufaika na urasimishaji waliishukuru MKURABITA kwa kuishirikiana na Halmashauri ya Mji kuchagua eneo lao kama eneo darasa katika kuwajengea uwezo. Kwa pamoja Mji waliahidi kuzitumia hati hizo kiuchumi katika kukuza mitaji na kuboresha maisha yao.

Mradi wa urasimishaji katika Halmashauri ya Mji Babati ulianza katikamkipindi cha mwaka wa fedha 2013/2020 kwa lengo la kuijengea uwezo Halmashauri ya Mji Babati waweze kuanza na kuendeleza shughuli za urasimishaji wa ardhi. Zoezi hilo lilinanendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi Namba 4 ya Mwaka 1999. Matarajio ya mradi huu ni kurasimisha viwanja vipatavyo 1,000 zoezi ambalo bado linaendelea.

Mgeni Rasmi Bw. Mathias Mkumbo alimkabidhi hati miliki kwa mmoja wa wakazi wa Mtaa wa Nangara ziwani waliorasimisha viwanja vyao kupitia MKURABITA