Tanzania emblem

The United Republic of Tanzania

Property and Business Formalization Program

News

Wanamakanda Wilayani Bahi wafurahia kupata elimu ya matumizi ya Hati Miliki za Kimila


Kufuatia kukamilika kwa zoezi la uhakiki na urasimishaji wa mashamba katika kijiji cha Makanda, MKURABITA kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Bahi iliandaa mafunzo ya siku moja kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi ya Hati Miliki za Kimila katika kupata na kukuza mitaji.

Mafunzo hayo yalihudhuriwa na wananchi waliorasimisha mashaamba yao wapatao 350 katika Kijiji cha Msisi na Wananchi 500 katika kijiji cha Makanda. Watoa mada kutoka taasisi za fedha zikiwemo benki za NMB na CRDB walishiriki pamoja na wataalam wa Halmashauri kutoka Idara ya Maendeleo ya Jamii, Ushirika, Mifugo, Kilimo na Misitu.
Katika mafunzo hayo wanachi 25 walijiorodhesha kwa ajili ya kufungua akaunti ambapo wanachi watatu walijiorodhesha na kuaanza mchakato wa kupata mikopo kwa ajili ya shughuli za kilimo.
Kwa takriban mwezi mmoja MKURABITA kwa kushirikiana na Halmashauri ilitoa mafunzo kwa wataalam wa Walaya 12, Maafisa ughani saba (7) pamoja na wajumbe wa Kamati ya Uhakiki - VAC/VLUM 27 kutoka vijiji vya Makanda na Msisi.
Jumla ya mashamba 1,407 katika Kijiji cha Makanda na 1,550 katika Kijiji cha Msisi yamepimwa. Kiasi cha Shilingi 2,571,600/= kimepokelewa katika kijiji cha Makanda ikiwa ni gharama ya usajili wa Hati Miliki. Jumla ya Shilingi 1,850,750/= zimekusanywa katika kijiji cha Msisi kwa ajili ya gharama ya usajili wa hati kutoka kwa wananchi waliorasimisha mashamba yao ikiwa ni takwa la kisheria. Zoezi la upimaji linaendelea.