News
Wana Makanda na Msisi taarifa za Miliki zao zaingizwa kwenye mfumo wa kidigitali
Wataalam kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wapo Wilayani Bahi wakiendelea na zoezi la uingizaji wa taarifa zilizomo kwenye hati katika Mfumo wa mafaili kuingizwa kwenye mfumo wa kidigitali wa ILMIS.
Katika zoezi hili kwa Wilaya ya Bahi Hati Miliki za Kimili za wananchi wa Vijiji vya Msisina Makanda zilizoandaliwa kwa Mujungu wa sheria ya Ardhi ya vijiji namba 5 ya mwaka 1999 zimekuwa sehemu ya taarifa zinazoingizwa kwenye mfumo huu Kama ilivyo kwa Hati Miliki zilizoandaliwa kwa Sheria ya Ardhi Namba 4 ya mwaka 1999.
Wataalam wa zoezi hili linaloendelea katika mikoa yote Tanzania Bara, wanatarajia kuwepo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kwa takriban wiki mbili. Aidha, uhakiki na uchapishaji wa Hati Miliki za Kimila kwa wananchi wa Msisi na Makanda inaendelea ambapo Hati zipatazo 1000 zimehakikiwa na kuchapishwa, ambapo Hati Miliki zipatazo 550 zimesajiliwa.