Tanzania emblem

The United Republic of Tanzania

Property and Business Formalization Program

News

UTOAJI HATI ZA VIWANJA HALMASHAURI YA MJI WA MAFINGA


Jumla ya Viwanja 1305 vimepimwa katika Kata ya Upendo na Hati Miliki 680 zimelipiwa Ada na Wananchi katika Mpango wa MKURABITA na jumla ya Shilingi milioni 75 zimetumika katika Mradi huo ambapo Serikali imegharamia kupanga na Kupima viwanja na wananchi kugharamia Ada Za umilikishaji pekee.

Akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Lumwago MRATIBU WA MPANGO WA MKURABITA CPA DK. Seraphia Mgembe amesema Lengo la Mpango ni kuhakikisha wananchi wanamiliki Uchumi wao kwa kuwa na Hati ambazo zinasaidia kuondoa migogoro ya ardhi na Kukuza uchumi wa wananchi wanyonge.

Akisoma Taarifa ya Mpango huo Ndugu Rajab Bogwa Afisa Mipango Miji wa Mji Mafinga amesema Lengo lilikuwa kupima viwanja 1000 lakini vimepimwa viwanja 1305 na kuvuka lengo hivyo kuhamasisha wananchi kulipia Ada za Umilikishwaji kwani Umiliki una faida nyingi ikiwemo kupata mikopo na kupunguza migogoro ya ardhi.

Akizungumza wakati wa kutoa Hati za Mfano kwa wananchi wa Mtaa wa Lumwago Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Saad Mtambule amesema Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan inajali sana wananchi wake kwani inagharamia kupanga na kupima ardhi na wananchi wanalipa tu Ada ya umiliki.

“ wananchi Hati miliki zilizolipiwa ni 680 Serikali imegharamia kupima na kupanga mlipie mchukue Hati zenu. Lengo la Serikali ni kuleta Maendeleo kwa wananchi wake .

Naye Diwani wa Kata ya Lumwago Mheshimiwa Michael Msite ameshukuru sana Mpango wa MKURABITA na Halmashauri ya Mji Mafinga kwa kuleta Mpango huo katika Kata yake ambapo wananchi wataondokana na Migogoro ya Ardhi na kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja.

Ugawaji wa hati za Mfano umeshughudiwa na Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Iringa, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mheshimiwa Regnant Kivinge, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Bi Happiness Laizer, waheshimiwa Madiwani, wataalamu ngazi ya Mkoa na Halmashauri, Waandishi wa Habari na wananchi wa Kata ya Upendo Mtaa wa Lumwago.