News
MRADI WA KUJENGA UWEZO NA KURASIMISHA RASILIMALI ARDHI ZA VIJIJI VYA MITEMA NA CHILANGALA KATIKA HALMASHAURI YA NEWALA
Ofisi ya Rais – MKURABITA imezindua mradi wa urasimishaji ardhi za wakulima wa vijiji vya Mitema naChilanga ratarehe 6 Aprili, 2022 kwa kutambulisha kwa Kamati Tendaji ya Wilaya, Halmashauri ya Kijiji na wananchi wa Mitema kwa kutoa elimu, uhamasishaji na mchakato wa utaratibu wa zoezi la urasimishaji na kujenga uwezo.
Mradi huu utashirikisha wataalam wa Kamati Shirikishi ya Mpango wa Matumizi Bora ya Wilaya kama watekelezaji, wajumbe wa Kamati ya uhakiki wa maslahi ya ardhi pamoja na Halmashauri ya Kijiji cha Mitema na Chilangala ambao watashiriki moja kwa moja kuanzia mwanzo mpaka mwisho.
Upimaji wa mashamba takribani 2,100 unatarajia kuanza jumatatu ya tarehe 11 Aprili, 2022 na kuendelea kwasiku 21