Tanzania emblem

The United Republic of Tanzania

Property and Business Formalization Program

News

Mkurugenzi wa Urasimishaji Ardhi na Biashara aguswa na hamasa ya wananchi wa Kijiji cha Makanda na Msisi wilayani Bahi


Bi Jane Lyimo Mkurugenzi wa Urasimishaji ardhi na Biashara kutoka MKURABITA, alipata fursa ya kutembelea Halmashauri ya Wilaya ya Bahi katika vijiji vya Makanda na Msisi kujionea jinsi mradi wa urasimishaji ardhi vijijini unavyotekelezwa.Akiwa uwandani alionana na uongozi wa vijiji vya Msisi na Makanda ambapo alielezwa jinsi wananchi walivyohamasika na kuendelea kujitokeza kwa wingi kuomba warasimishiwe mashamba yao. Walieleza hofu iliyopo miongoni mwa wananchi kuwa muda uliopangwa ni mfupi hivyo wengi wakihofia mashamba yao kutofikiwa na mradi huu.

Mkurugenzi alishuhudia wananchi wa Kijiji cha Makanda wakiwa wanaendelea kumiminika kujaza fomu za maombi ya kuandaliwa hati miliki na wengine wakiendelea kufanya malipo ya usajili kwa ajili ya hati zao zitakapoandaliwa. Hivyo aliwapongeza viongozi kwa jitihada na hamasa waliyoifanya na kuwezesha wananchi kujitokeza kwa wingi. Aliwatoa hofu na kuwahakikishia kwamba zoezi hili litakuwa endelevu ndio maana MKURABITA imejenga uwezo wa wataalam katika ngazi ya Wilaya, kata na baadhi ya vijana kutoka katika vijiji husika ili uhitaji unapojitokeza waweze kusaidia kuwapiamia wale waliobaki hata baada ya wataalam wa Timu ya MKURABITA kuondoka.

Akiwa katika Kijiji cha Msisi alishuhudia wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji wakiwa na wajumbe wa Kamati ya Kjiji cha Msisi wakiendelea na zoezi la kukamilisha uandaaji wa Mpango wa Matumizi ya Ardhi. Mwenyekiti wa Kijijialimweleza Mkurugenzi jinsi mchakato ulivyofanyika hadi hatu ya kuandaa sheria ndogo za kusimamia utekelezaji wa Mpango huo ulioandaliwa, Pia alimweleza kuwa Mpango huo umeandaliwa tayari kwa ajili ya mawasilisho katika Mkutano wa Kijiji ili wananchi waweze kuupitisha sambamaba na sheria ndogo zilizoandaliwa pamoja na ratiba ya kuanza kwa uhakiki wa mashamba ya wananchi.