Tanzania emblem

The United Republic of Tanzania

Property and Business Formalization Program

News

MKURABITA yatambulisha Mradi wa Urasimishaji Ardhi Vijijini wilayani Bahi.


Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Tarehe 21 /03/2022 umetambulisha mradi wa urasimishaji ardhi vijijini kwa Uongozi wa Wilaya ya Bahi.

Katika kutambulisha Mradi huo MKURABITA Bw. Anthony katiak kutambulisha mradi huo kiongozi wa Timu ya MKURABITA alikutana na wajumbe wa Kamati ya Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, ambapo walielezwa kuhusu shughuli za MKURABITA na mradi wa urasimishaji ardhi vijijini unalotarajiwa kutekelezwa katika Halmashauri hiyo.

Meneja wa Urasimishaji Ardhi Vijijini kutoka MKURABITA Bw. Anthon Temu aliwaeleza wajumbe kuwa lengo la Mradi huu ni kuwajengea uwezo Halmashauri ili iwe na mchakato endelevu wa urasimishaji ardhi vijijini kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya Vijiji Namba 5 ya Mwaka 1999

Katika kujenga uwezo, walielezwa kwamba MKURABITA itatoa mafunzo ya nadharia kwa timu ya watalaam wa Halmashauri pamoja na mafunzo ya vitendo katika vijiji viwili vya Msisi na Makanda. Katika zoezi hili pia MKURABITA itaweshesha ujenzi wa Ofisi ya Msajala ya Ardhi ya Kijiji cha Msisi na Kijiji cha Makanda ikiwa ni hitaji la kisheria.

Uongozi wa Wilaya ya Bahi umeishukuru MKURABITA kwa uamuzi huo na kuwahikikishia ushirikiano wake kwa MKURABITA wakati wa utekelezaji wa Mradi huu. Nao wananchi wa Kijiji cha Msisi wamekiri kuwa Serikali kupitia MKURABITA imekuja kuwainua kiuchumi wawe matajiri kupitia ardhi yao.

Tangu kuanzishwa kwa MKURABITA mwaka 2004, Halmashauri za wilaya 60 zimejengewa uwezo. Halmashauri 25 zimeonesha kupiga hatua kubwa zaidi katika kuhakikisha urasimishaji ardhi vijijini unakuwa endelevu katika Halmashauri zao.