Tanzania emblem

The United Republic of Tanzania

Property and Business Formalization Program

News

MKURABITA yashirikiana na Halmashauri ya Mji wa Tarime kujenga Kituo Jumuishi cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara


Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mji wa Tarime wapo katika hatua za kukamilisha ujenzi wa Kituo Jumuishi cha Urasmishaji na Uendelezaji Biashara katika Mji wa Tarime.

Lengo la kuanzisha Kituo Jumuishi cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara katika Halmashauri ya Mji wa Tarime ni kurahisisha huduma ya kurasimisha Biashara kwa gharama nafuu na uwezeshwaji wa Mitaji.

Uwepo wa Kituo Jumuishi cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara katika Halmashauri ya Mji wa Tarime unatarajiwa kuleta hamasa kwa Wafanyabiashara na Waendesha Bodaboda na Bajaji kwenda kupata huduma za Urasimishaji na Uendelezaji Biashara katika eneo moja.