Tanzania emblem

The United Republic of Tanzania

Property and Business Formalization Program

News

MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAFANYABIASHARA NA WAENDESHA BODA BODA NA BAJAJI WA HALMASHAURI YA MJI WA TARIME


Kuanzia tarehe 25 Aprili, 2022 MKURABITA kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mji wa Tarime na Wadau wa Urasimishaji kutoka taasisi za Umma na binafsi zikiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Sirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Sirika la Kuhudumia Viwanda vidogo vidogo (SIDO), Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Jeshi la Polisi, Taasisi za Fedha (Mabenki), Chama cha Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) na Chama cha Waendesha Bodaboda na Bajaji Wilaya ya Tarime wataandaa mafunzo ya Urasimishaji na Uendelezaji Biashara kwa Wafanyabiashara wadogo na wa kati pamoja na Waendesha Bodaboda na Bajaji wa Mji wa Tarimie. Maandalizi yatahusisha kukusanya takwimu za Wafanyabiashara na Wendesha Bodaboda na Bajaji takribani 2,000 kutoka katika Kata na Mitaa ya Mji wa Tarime.

Zoezi la kukusanya na kuchaka taarifa litafanyika kwa siku 10 kuanzia tarehe 25 Aprili hadi tarehe 5 Mei, 2022. Taarifa zitakazokusanywa zitasaidia kujua mahitaji halisi na hivyo kuwawezesha Wadau wa Urasimishaji kuandaa na kuweka mipango ya mafunzo ya kuwajengea uwezo Wafanyabiasha na waendesha Boda boda na Bajaji wa Mji wa Tarime. Kikao cha Wadau kwa ajili ya kuandaa mafunzo kitafanyika tarehe 6 Mei, 2022 mjini Tarime.

Mafunzo kwa Wafanyabiashara na Waendesha Boda boda na Baji yanatarajiwa kuanza tarehe 9 Mei hadi tarehe 13 Mei, 2022. Baada ya mafunzo, zoezi la usajili wa Biashara na uwezeshaji Mitaji litaendelea kuanzia tarehe 16 Mei, 2022.