Tanzania emblem

The United Republic of Tanzania

Property and Business Formalization Program

News

URASIMISHAJI BIASHARA SUMBAWANGA


MKURABITA kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga pamoja na wadau wa Urasimishaji na Uendelezaji Biashara wametoa mafunzo ya urasimishaji na uendelezaji biashara kwa wafanyabiashara wa Mjini humo. Wakufunzi walieleza kwa kina juu ya umuhimu wa urasimishaji katika ukuaji wa mitaji, utunzaji wa kumbukumbu za biashara, ulipaji sahihi wa kodi ya mapato, uwekaji wa akiba katika mifuko ya pension pamoja na umuhimu wa kukata bima za biashara. Suala la uanzishaji wa viwanda pia ulielezwa.

Wadau walioshirikiana na MKURABITA kutoa mafunzo hayo ni pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), na taasis za fedha wakiwemo benki za NMB, CRDB na NBC.