Tanzania emblem

The United Republic of Tanzania

Property and Business Formalization Program

News

MKURABITA YASHIRIKI MAONESHO YA TANO (5) YA MIFUKO NA TAASISI ZA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI, MOROGORO-UWANJA WA JAMHURI


Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Bisashara za wanyonge Tanzania (MKURABITA) imekuwa miongoni mwa wadau wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji ambalo limeandaa maonesho ya tano (5) ya mifuko na taasisi za uwezeshaji wananchi kiuchumi.Maonesho haya yamedhaminiwa na TACT na kuratibiwa na Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi katika Viwanja vya Jamhuri Morogoro. Maonesho yameshirikisha taasisi zipatazo mia moja zinazohusikana masuala ya uwezeshaji wa wananchi kiuchumi yamezinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Martin Shigella kwa niaba ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Katika maonesho haya MKURABITA imeshiriki kwa mara ya kwanza ikiwa ni Progamu mdau na mshirika wa ajenda ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia urasimishaji rasilimali ardhi na biashara, MKURABITA imeshiriki ikiwa pamoja na wadau wa urasimshaji biashara na wanufaika wake kupitia dhana ya Kituo Jumuishi cha Urasimishaji na Uendelezaji biashara cha Manispaa ya Morogoro.Aidha, Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo – SIDO na Mamlaka ya Mapato Tanzania - TRA walitarajiwa kushiriki katika banda la MKURABITA lakini hawakuweza kufanya hivyo kutokana kuwepo kwa mabanda yao.

Katika Maonesho haya MKURABITA ilipata fursa ya kutambulisha Mpango huu pamoja na majukumu ya msingi yanayotekelezwa hapa nchini, Pia ilipata fursa ya kutembelewa na Mgeni rasmi katika banda lake, ambapo aliipongeza MKURABITA kwa kazi zinazoendeleapamoja na ubunifu wake uliowezesha kuanzishwa kwa kituojumuishi cha urasimishaji na uendelezaji biashara pamoja na Ardhi kilichopo Mafiga, Manispaa ya Morogoro. Pia alipongeza MKURABITA kwa kuibua wanyonge kuwa mamilionea wanao zalisha na kuwa sehemu ya umiliki wa uchumi hapa nchini.

Maonesho haya ambayo yamefunguliwa rasmi tarehe 9 Mei 2022 yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 14 Mei 2022 lengo ikiwa ni kuwwezesha wananchi kufahamu juu ya mifuko na program mbalimbali hapa nchini zinazotoa huduma za kuwezesha kiuchumi. Aidha maonesho haya yanatoa nafasi kwa wajasiriamali na watoa huduma za uwezeshaji wananchi kiuchumi kubadilishana uzoefu na kujitangaza zaidi pamoja na kupanua wigo wa wateja na wadau hapa nchini,


KAULI MBIU:

“UCHUMI IMARA KWA MAENDELEO ENDELEVU”