Tanzania emblem

The United Republic of Tanzania

Property and Business Formalization Program

How Do I?

Urban Property Formalization

 • Ili uweze kurasimisha eneo la Ardhi yako Mjini kwa mujibu wa Sheria Namba 4 ya Ardhi ya Mwaka 1999 yakupasa kufahamu na kuzingatia yafuatayo:-
  • Kujua kama eneo lako lipo katika Mipangomiji ya eneo husika na lina mchoro wa Mipangomiji
  • Kujua eneo lako limepangwa kwa matumizi husika ambayo yaweza kuwa ni makazi pekee, Makazi na biashara, Biashara pekee au matumizi mengine kama vile viwanda vidogo, kilimo cha mjini au viwanda vikubwa
  • Kutambua mipaka ya eneo lako la asili ambapo zoezi hili hufanywa kwa kutumia vifaa vya kitaalam kama vile Handheld GPS au RTK
  • Kujaza fomu ya maombi ya kupimiwa eneo lako na kupewa hati miliki kutoka ofisi za ardhi zilizopo katika Halmashauri yako
  • Eneo kupimwa na Wataalamu wa Upimaji walioidhinishwa na Mamlaka husika.
  • Kufanya malipo ya Ankara kulingana na ukubwa wa eneo lako.
  • Kuandaa, kusajili na kukabidhi Hati wamiliki wa viwanja.