Tanzania emblem

The United Republic of Tanzania

Property and Business Formalization Program

How Do I?

To Formalize Rural Property/ Land

Ili uweze kurasimisha ardhi yako kijijini kwa mujibu wa Sheria Namba 5 ya Ardhi ya Kijiji ya Mwaka 1999 zingatia yafuatayo:-

  • Hakikisha Ardhi unayotaka Kurasimisha ipo katika Kijiji chenye Cheti cha Ardhi ya Kijiji
  • Hikikisha Kijiji kina Mpango wa Matumizi ya Ardhi ya Kijiji
  • Hakikisha ardhi yako haina mgogoro wa mipaka na umiliki
  • Jaza fomu ya maombi ya kupimiwa Ardhi yako na kuwasilisha Ofisi ya Kijiji ilipo Ardhi yako.
  • Hakikisha maombi yako ya kupimiwa Ardhi yameidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji
  • Ardhi yako itapimwa na Wataalam wa Upimaji walioidhinishwa na Mamlaka husika
  • Utafanya malipo ya Ankara kulingana na ukubwa wa eneo lako.
  • Uandaaji na Usajili wa Hati za Haki Milki za Kimila utafanyika na Mmiliki kupewa nakala moja ya Hati na nakala nyingine kutunzwa katika Masjala ya Ardhi ya Kijiji na nyingine katika Masjala ya Ardhi ya Wilaya.