Tanzania emblem

The United Republic of Tanzania

Property and Business Formalization Program

Events

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama kufanya ziara ya siku mbili (2) Mjini Unguja, Zanzibar


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama anatarajia kufanya ziara ya siku mbili (2) Mjini Unguja, Zanzibar kuanzia tarehe 24 Januari hadi 26 Januari 2023. Lengo la ziara hii ni kujionea maendeleo ya utekelezaji wa shughuli za urasimishaji Zanzibar.

Akiwa Zanzibar, Mhe. Mhagama atapokea taarifa kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar kupitia Tume ya Mipango yenye dhamana ya uratibu wa shughuli za MKURABITA Zanzibar. Mhe. Waziri atapata fursa ya kutembelea maeneo ya miradi iliyopo Mjini Unguja ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Ofisi ya Masjala ya Ardhi pamoja na uanzishwaji wa Vituo Jumuishi vya Urasimishaji na Uendelezaji Biashara.

Pamoja na mambo mengine, Mhe. Waziri atatoa Hati Milki kwa wananchi wa Shehia ya Meya. Aidha, Mhe. Waziri atakutana na kuzungumza na baadhi ya wadau na wanufaika wa urasimishaji ardhi na biashara ili kusikia shuhuda zao juu ya tija na manufaa ya kiuchumi yaliyopatikana kutokana na urasimishaji.

MKURABITA inatekeleza shughuli za urasimishaji Tanzania Zanzibar kwa kushirikiana na Tume ya Mipango, Zanzibar pamoja na Wizara za Kisekta ikiwemo Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi pamoja na Wizaa ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda. Wadau wengine ni pamoja na Halmashauri, Taasisi za fedha,mifuko ya jamii, Mamlaka ya Mapato (Tanzania na Zanzibar) shirika la viwango, ZIPA na mamlaka inayosimamia usajili wa biashara (Zanzibar Business and Property Registration Agency – BPRA).