Uhusiano wa MKURABITA na Mikakati ya Kitaifa – MKURABITA пумб погасить кредит онлайн онлайн кредит на карту без фото паспорта украина кредиты онлайн без отказов кредит онлайн на карту без отказа и звонков круглосуточно кредит без отказа онлайн

inapakia

Uhusiano wa MKURABITA na Mikakati ya Kitaifa

MKURABITA itatekelezwa kupitia mfumo wa serikali kuu na serikali za mitaa ili kuepuka urudufishaji wa jitihada na gharama au maganyiko usio wa lazima. Mipango ya urasimishaji itaenda sambamba na mipango na mikakati mingine ya maendeleo ili kwa pamoja vielekeze nguvu ya pamoja katika kupunguza umaskini na hivyo kuepuka migongano katika mipango ya maendeleo inayofanana.

MKURABITA katika muktadha wa MKUKUTA, MKUZA na Mipango Mingine ya Kitaifa

MKUKUTA na MKUZA ni mikakati ya kitaifa inayolenga kukuza uchumi na kuondoa umaskini. Dhana ya MKURABITA katika muktadha wa mikakati hiyo miwili inatoa mbinu za kukuza uchumi na kuondoa umaskini Tanzania Bara na Visiwani. Uhakiki wa uhusiano wa MKURABITA katika kufikia malengo na matarajio ya MKUKUTA na MKUZA unaonyesha kuwa utekelezaji wa maeneno makuu ya Mpango wa Urasimishaji sambamba na mipango mingine vitachangia kwa namna moja au nyingine kaitka kufikia malengo ya MKUKUTA na MKUZA. Kwa mfano, kuwezeshwa kwa wajasiriamali wadogo na wa kati kama sehemu ya sekta binafsi inaonyesha wazi kwa kiasi kikubwa kutapunguza umaskini hasa kwa kipato.

MKURABITA itatekelezwa kupitia muundo wa vyombo vya serikali vilivyopo na hasa vile vya mfumo wa serikali za mitaa. Mabadiliko ya muundo wa kitaasisi yanayotarajiwa kutokea kama matokeo ya mbaroesho vitaonishwa kikamilifu na Mpango wa Maboresho ya Serikali za Mitaa.

Utekelezaji wa mipango mahsusi ya MKURABITA utaunganishwa katika sekta muhimu kama vile sekta ya kilimo na hasa katika Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo, Mpango wa Kuendeleza Wajasiriamali Wadogo na wa Kati, Mpango wa Maboresho ya Sekta ya Sheria, Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Sheria, na mipango mingine ya maendeleo ianyosimamiwa na jamii.

Maendeleo ya sekta binafsi ni njia mojawapo ya kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya kupunguza umaskini. Sekta binafsi pia itanufaika kwa kupata haki ya kumiliki mali kisheria na kwa kupanua wigo wa ujasiriamali nchini.

© Hakimiliki 2018  MKURABITA. Haki Zote Zimehifadhiwa.