inapakia

MKURABITA ni Nini?

Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania maarufu kama “MKURABITA” ni miongoni mwa jitihada za serikali katika kuwezesha jamii kiuchumi. MKURABITA imeanzishwa na Serikali ya Tanzania mwaka 2004 kwa lengo la kuwapa nguvu ya kiuchumi wananchi kwa kuwaongezea uwezo wa kumiliki na kufanya biashara katika mfumo rasmi unaozingatia utawala wa sheria.  Mpango huu unasimamiwa na kuratibiwa na Ofisi ya Rais, Ikulu.   

 

MKURABITA ni sehemu ya Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania (MKUKUTA) na Mkakati wa Kuondoa Umasikini Zanzibar (MKUZA), ukilenga kuwawezesha walengwa kutumia rasilimali na biashara zao zilizo rasimishwa katika kujipatia mitaji, soko pana na fursa zingine zinazopatikana katika sekta rasmi na hivyo kupunguza umaskini wa kipato.

Tovuti hii ni lango linalolinalowezesha kupata taarifa muhimu na za kina kuhusu ajenda ya uwezeshaji kiuchumi kupitia urasimishaji rasilimali na biashara na kuendeleza dhana ya utawala wa sheria nguzo muhimu katika ukuzaji wa mitaji na utawala bora.

Aidha, kwa kutembelea tovuti yetu ya www.mkurabita.go.tz umma kwa ujumla unaweza kupata taarifa mbalimbali ikiwemo chimbuko la uwepo wa sekta isiyo rasmi nchini, jitihada zinazofanywa na serikali kutatua kukithiri kwa sekta isiyo rasmi na kuimarisha umoja wa kitaifa na uchumi unaojumuisha jamii yote.

Pia maelezo juu ya hatua muhimu katika urasimishaji rasilimali na biashara, manufaa na matokeo yanayotarajiwa kutoka MKURABITA, machapisho pamoja na taarifa za wadau katika ajenda ya uwezeshaji kiuchumi. Wote mnakaribishwa kwa magwiji wa maboresho katika urasimishaji na mfurahie kutembelea tovuti hii.

© Hakimiliki 2018  MKURABITA. Haki Zote Zimehifadhiwa.