MKURABITA kwa Muhtasari – MKURABITA кредит наличными онлайн на карту онлайн кредит на карту без фото паспорта украина finme кредит онлайн кредит онлайн без отказов на карту банк финансы и кредит онлайн

inapakia

MKURABITA kwa Muhtasari

Utangulizi

Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania maarufu kama “MKURABITA” ni miongoni mwa jitihada za serikali katika kuwezesha jamii kiuchumi. MKURABITA imeanzishwa na Serikali ya Tanzania mwaka 2004 kwa lengo la kuwapa nguvu ya kiuchumi wananchi kwa kuwaongezea uwezo wa kumiliki na kufanya biashara katika mfumo rasmi unaozingatia utawala wa sheria. Mpango huu unasimamiwa na kuratibiwa na Ofisi ya Rais, Ikulu.

MKURABITA ni sehemu ya Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania (MKUKUTA) na Mkakati wa Kuondoa Umasikini Zanzibar (MKUZA), ukilenga kuwawezesha walengwa kutumia rasilimali na biashara zao zilizo rasimishwa katika kujipatia mitaji, soko pana na fursa zingine zinazopatikana katika sekta rasmi na hivyo kupunguza umaskini wa kipato.

Tovuti hii ni lango linalolinalowezesha kupata taarifa muhimu na za kina kuhusu ajenda ya uwezeshaji kiuchumi kupitia urasimishaji rasilimali na biashara na kuendeleza dhana ya utawala wa sheria nguzo muhimu katika ukuzaji wa mitaji na utawala bora.

Aidha, kwa kutembelea tovuti yetu ya www.mkurabita.go.tz umma kwa ujumla unaweza kupata taarifa mbalimbali ikiwemo chimbuko la uwepo wa sekta isiyo rasmi nchini, jitihada zinazofanywa na serikali kutatua kukithiri kwa sekta isiyo rasmi na kuimarisha umoja wa kitaifa na uchumi unaojumuisha jamii yote.

Pia maelezo juu ya hatua muhimu katika urasimishaji rasilimali na biashara, manufaa na matokeo yanayotarajiwa kutoka MKURABITA, machapisho pamoja na taarifa za wadau katika ajenda ya uwezeshaji kiuchumi. Wote mnakaribishwa kwa magwiji wa maboresho katika urasimishaji na mfurahie kutembelea tovuti hii.

 

Kuanzishwa kwa MKURABITA

Semina ya siku mbili ya uhamasishaji kwa viongozi wakuu wa serikali na mashirika mbalimbali juu ya Haki Miliki ilifanyika katika ukumbi wa Karimjee, mnamo Septemba 8 – 9, 2003.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa semina siku ya kwanza. Naye Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu, Mheshimiwa Cleopa Davidi Msuya alishika uenyekiti wa semina hii siku ya pili.

Miongoni mwa wajumbe waliohudhuria ni pamoja na mawaziri na manaibu mawaziri wote, wakuu wa mikoa, makatibu wakuu, maafisa wandamizi serikalini, wakuu wa taasisi za umma, mashirika ya kijamii pamoja na waandishi wa habari.

Aidha, semina iliandaliwa kwa lengo la kuwahamasisha na kutoa ufahamu kwa Uongozi wa Tanzania juu ya uwiano uliopo baina ya haki miliki kwa rasilimali zilizo rasmi na kukua kwa mitaji pamoja na kuongeza pato katika muktadha wa usawa na maendeleo ya kiuchumi yanayojumuisha wengi.

Dr. Hernando de Soto, Rais wa Taasisi ya ‘Institute for Liberty and Democracy (ILD)’ kutoka Peru, aliwasilisha mada kuhusu uzoefu wa muundo wa taasisi hiyo kwenye urasimishaji wa rasilimali na biashara na katika kuunda mfumo mmoja unaowaunganisha wamiliki na haki miliki za rasilimali na biashara.

Bw. John Schjelderup Olaisen, Mkurugenzi Mtendaji wa Norway Registers Development naye aliwasilisha ripoti ya Warsha ya Urasimishaji wa Rasilimali Tanzania iliyofanyika Mei 2003.

Katika semina hii Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin Mkapa, alitoa hutuba ya ufunguzi iliyosisimua wengi kwa kusisitiza umuhimu na manufaa ya urasimishaji wa rasilimali na biashara katika kuwawezesha Watanzania walio wengi kiuchumi na kupunguza umasikini. Dhana hii pia iliainishwa vizuri katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 1995 na 2000.
Katika siku mbili za majadiliano, uongozi wa kitaifa ulitoa azimio la kuanzishwa kwa mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara zisizo rasmi kwa lengo na madhumuni ya kuwawezesha wamiliki wa mali hizi kushiriki katika uchumi rasmi unaosimamiwa na utawala wa sheria. Hii ni pamoja na kuzitumia mali zao zilizokwisha rasimishwa kama dhamana katika kupata mikopo na fursa zinginezo zilizoko katika uchumi wa soko.

Pia Uongozi uliamua kutumia muundo wa ILD wenye awamu nne za utekelezaji ili kupata huduma ya ushauri kutoka katika taasisi hii katika awamu mbili za awali.
Utekelezaji wa awamu mbili za mwanzo ulianza Novemba, 2004 na ulipangwa uwe umekamilika katika kipindi cha miezi 31 na baadaye (Julai 2007). Kutokana na mabadiliko kadhaa utaratibu wa utekelezaii wa awamu hizi mbili (tathmini ya sekta isiyo Rasmi na Uandaajiwa Maboresho) Ulikamilika Julai 2008.

Matokeo ya utekelezaji wa awamu hizi mbili yanapatikana katika Nyaraka kama:
1. Report on the Diagnosis – provided in the following seven volumes:-

 1.  Volume 1 – Executive Summary
 2. Volume II – The Legal Economy: Its Archetypes and size
 3. Volume III – The Legal Economy: Its institutions and costs
 4. Volume IV – Barriers to using Property and Doing Business nationwide
 5. Volume VA – Step by Step: The People’s experience of Legal Procedures (Real Estate Procedures)
 6. Volume VB – Step by Step: The People’s experience of Legal Procedure (Business procedures).
 7. Volume VI – Supporting Documents

2. Institutional and Legal Reform Proposals provided in seven volumes as follows:-

 1. Volume I – Executive Summary
 2. Volume II – Property Formalization – Reform Outlines and Packages for Tanzania Mainland.
 3. Volume III – Property Formalization Reform Outlines and Packages for Zanzibar
 4. Volume IV – Business Formalization Reform Outlines and Packages for Mainland Tanzania.
 5. Volume V – Business Formalization Outlines and Packages for Zanzibar.
 6. Volume VI – Institutional Arrangements
 7. Volume VII – Work Plan, Monitoring and Evaluation Framework and Cost Benefit Analysis.

Utekelezaji wa Awamu ya Tatu unaendelea, ambao umejikita zaidi katika utekelezaji wa sheria na mapendekezo mbalimbali ya kitaasisisi yaliyoandaliwa katika Awamu ya Pili ili kusukuma mbele mchakato wa urasimishsaji wa rasilimali na biashara katika sekta isiyo rasmi. Pamoja na Mpango wa utekelezaji wa miaka kumi.

Awamu ya Nne kwa kiasi kikubwa inakwenda sambamba na utekelezaji wa Awamu ya Tatu katika kuzinganisha na mitaji rasilimali na biashara zilizorasimishwa na fursa nyinginezo za kiuchumi. Aidha, Awamu ya Nne hii inajumuisha mchakato mzima wa kuweka na kutekeleza mapendekezo yanakayoziunganisha rasilimalina biashara zilizorasimishwa na masoko rasmi katika ngazi ya taifa na kimataifa ili kuwezesha mali zilizorasimishwa kutumika kwa dhamana kwa lengo la kuongeza mitaji na pato.

Kitengo cha Uongozi cha MKURABITA kinaratibu na kusimamia ujengaji uwezo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuwezesha upatikanaji wa rasilimali zinazohitajika katika kufikia malengo na matokeo yanayotarajiwa pamoja na kusimamia na maendeleo ya utekelezaji na ushauri wa kitaalam. Serikali za Mitaa ambao ndio watekelezaji wa shughuli za urasimishaji na wizara za kisekta, zinahusika zaidi na uboreshaji wa sheria na maboresho ya kitaasisi yenye lengo la kuanzisha kwa mfumo mmoja wa kitaifa wenye kusimamia haki miliki za rasilimali na biashara.

Mapendekezo ya Maboresho na shughuli za utekelezaji ni shughuli ya kudumu itakayowezesha kuwepo kwa mabadiliko kadri itakavyokuwa na yanatekelezwa kulingana na mahitaji na matakwa ya walengwa wa Mpango huu.

© Hakimiliki 2018  MKURABITA. Haki Zote Zimehifadhiwa.