Manufaa na Mategemeo Yanayotarajiwa – MKURABITA кредит на банковскую карту онлайн онлайн займ россия онлайн кредит на карту украина кредит 24 онлайн финансы и кредит онлайн кредит без отказа онлайн

inapakia

Manufaa na Mategemeo Yanayotarajiwa

Ushahidi wa Faida za Kiuchumi na Kijamii

Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania unatarajiwa kuleta mafanikio makubwa katika uchumi wan chi. Ushahidi umeonyesha kuwa kuna mafanikio makubwa ya kiuchumi na uboreshaji wa hali ya maisha ya wanyonge katika nchi kadhaa ambapo mango kama huu umeketekelezwa kama mfano:

 • Kwa kuwekeza dola za kimarekani million 18.2 katika Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara nchini Peru katika ya mwaka 1982 ana 1996 wanyonge walipata Dola za Kimarekani Bilioni 9.4 katika faida hali kati ya mwaka 1991na 2002 ambayo ni sawa na wastani wa ongezeko la pato kwa Asilimia 173.
 • Nchini Japan matokeo ya maboresho yaliyolenga kuwapatia raia wa kipato cha chini haki ya kumiliki mali mwaka 1946 yalivuka malengo yaliyotarajiwa kwa kiwango kikubwa. Katika kipindi cha miaka mine tu asilimia hamsini (50%) ya Ardhi ilirashimishwa na kufikia mwaka 1952 (miaka sita baadaye) pato la mkulima liliongezeka kwa asilimia themanini 80%)
 • Nchini Taiwan, mashamba mapya ya Mpunga wenye hati miliki yaliongeza Uzalishaji kwa asilimia sitini (60%) kati ya mwaka 1953 na 1963 wakati pato la wamiliki wao liliongezeka kwa asilimia mia moja hamsini (150%)
 • Vietnam ya Kusini ambapo kati ya 1993 na 1998 serikali ilitoa hati miliki za miaka 20 na 50 kwa kilimo cha mavuno ya mwaka mmoja na zaidi; Uzalishaji kwa mwaka uliongezeka kwa asilimia thelathini na tatu nukata nne (33.4%) pale wakulima walipopatiwa haki hizi na watu wanaoishi chini ya kiwango cha umaskini walipungua kutoka asilimia 58 mapaka asilimia37.
 • Nchini China urasimishaji wa rasilimali uliofanyika katika ya mwaka 1980 mpaka 1990 ulisaidia kuongeza kukua kwa pato la kilimo kwa asilimia 86. mafanikio haya hayajumuishi maboresho maalum kwama vile mapinduzi ya kilimo.
 • Utafiti uliofanyika kwa miaka mitatu karibuni katika mashamba ya “kijamaa” huko Ukranine umeonesha kuwa wanachama milioni tatu waliopewa hati miliki walipata ongezeko la kipato la asilimia 81 ikilinganishwa na wanachama milioni 3.7 ambao hawakupata hati miliki.
 • Nchini Urusi, ambapo asilimia tano tu (5%) ya Ardhi ya kilimo ina hati miliki zilizotolewa kwa wamiliki wake, Uzalishaji unaotokana na asilimia tano hii ni sawa na asilimia hamsini (50%) ya Uzalishaji wa kilimo wan chi nzima, na asilimia hamsini iliyobaki (50%) inazalishwa na Ardhi isiyo na hati miliki ambayo ni sawa na asilimia tisini na tano (95%)

Mafanikio ya Urasimishaji Yanayotarajiwa Nchini Tanzania

Nchini Tanzania, mafanikio yafuatayo yanatarajiwa kaitka utekelezaji wa Mpango huu;

 • Kuboreka kwa mazingira ya biashara
 • Kuongeza umiliki wa rasilimali kisheria na upatikanaji wa mitaji kwa wenye rasilimali
 • Upanuzi wa sekta ya uchumi rasmi kwa kupunguza ukubwa wa sekta isiyo rasmi na kuwezesha wadau wake kutumia rasilimali zako kujipatia mitaji na kushiriki kikamilifu katika uchumi wa soko rasmi kitaifa na kimataifa
 • Kuongeza pato la serikali kutoka kwa walipa kodi wapya
 • Ukuaji wa uchumi na kupunguza uamskini wa kaya kupitia ushiriki wa wananchi Walio wengi katika sekta rasmi ya uchumi
 • Utawala bora kutokana na utoaji taarifa sahihi za mwenendo wa masoko, hali ya rasilimali na kiwango cha utawala wa kisheria

© Hakimiliki 2018  MKURABITA. Haki Zote Zimehifadhiwa.