Awamu ya Utekelezaji wa Maboresho ya Mapendekezo – MKURABITA срочный займ онлайн на карту украина металлоискатель в кредит онлайн кредиты на карту онлайн кредит на карточку приватбанка

inapakia

Awamu ya Utekelezaji wa Maboresho ya Mapendekezo

Awamu ya Tatu ya MKURABITA inajumuisha utekelezaji wa sheria na mapendekezo mbalimbali ya kitaasisisi yaliyoandaliwa katika Awamu ya Pili ili kusukuma mbele mchakato wa urasimishsaji wa rasilimali na biashra katika sekta isiyo rasmi. Awamu hii ilianza rasmi Julai 2008 na utekelezaji wake unafanywa katika mpango wa muda mfupi (mwaka mmoja), kati (miaka mitano) na mrefu (miaka kumi). Awamu hii pia inalenga kutekeleza kampeni za kuhamasisha urasimishaji wa rasilimali na biashra, kujenga muafaka, kuweka mfumo wa kupata mrejesho, pamoja na kuweka kitengo cha taifa cha kumbukumbu na utunzaji wa takwimu. Shughuli Nyingine zitakazojumuishwa katika awamu hii ni pamoja na;

  • Kurekebisha na kutunga sheria mpya ama kuweka taratibu ambazo zitarahisisha mchakato wa kurasimisha rasilimali na biashara kwa gahrama nafuu.
  • Kufanya maboresho ya sera mbalimbali zilizobainishwa, na kuimarisha vyombo vilivyoundwa na serikali ambavyo ni muhimu katika kurasimisha rasilimali na biashara katika ngazi ya serikali kuu na serikali za mitaa
  • Kuimarisha na kuanzisha miundombinu muhimu ya kitaasisi pamoja na kutoa mafunzo yanayohitajika kwa watendaji

Kujenga Muafaka Miongoni mwa Wadau

Mchakato wa kujenga muafaka miongoni mwa wadau na mazingira ya utekelezaji wa maboresho utafanyika kwa kutoa taarifa za MKURABITA na muafaka wake kwa ktumumia mbinu na vyombo mbalimbali vya habari. Taarifa hizi zitakuwa mahsusi kwa makundi na wadau mbalimbali katika jmii kama vile sekta isisyo rasmi, wafanyabiashra, mamlaka za kijadi, maofisa wa seriklai, na makundi mengine ambayo yanaweza kutoafikiana na mabadiliko. Mchakao huu utakuwa na mfumo wa kutoa taarifa nchi nzima kwa lengo la kujenga uelewa na muafaka katika maeneo ya mbadiliko na kupata mrejesho kutoka kw a wadau na jamii kwa ujumla.

Kutekeleza mapendekezo ya Maboresho ya Kisheria na Kitaasisi

Hatua hii inahusisha kuweka maboresho ya kisheria na kitasisi ambayo yalibainishwa kama sehemu ya urasimishaji na yale ambayo yanaonekana kuwa muhimu kuboreshwa kulingana na maoni ya wadau. Mchakato pia unahusisha na kupitiwa upya mapendekezo ya maboresho yanayotolewa na timu ya vikosi kazi maalum vya MKURABITA na wizara husika ili kupata ridhaa ya wizara za kisekta na hatimaye kupitishwa na Baraza la Mawaziri, kuandaa miswada na kupitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano au Baraza la Wawakilishi kwa upande wa Zanzibar. Sambamba na mchakato huu, ridhaa ya wizara na mamlaka husika zitatumika katika kufanya majaribio ya mapendekezo yaliyotolewa kabala ya Bunge au Baraza la Wawakilishi kupitisha sheria za kitaasisi kadiri ya muunda wake wa utekelezaji. Wakati wa majaribio uhalali wa sheria wa matokeo ya msingi ya urasimishaji utazingatiwa.
Utekelezaji wa Mapendekezo

Hatua hii itahusisha zaidi utekelezaji wa mchakato wa urasimishaji wa rasilimali na biashra katika ngazi ya serikali kuu na serikali za mitaa. Utekelezaji utazingatia sheria mpya na miundo mipya ya kitaasisi kama ilivyoafikiwa na wizara mbalimbali za kisekta. Mafunzo yatakayopatikana kuptia katika utekelezaji huu yatatumika kuboresha zaidi mapendekezo ya urasimishaji na kuimarisha vyombo na zana za mawasiliano ili kujenga muafaka juu ya mabadiliko yanahitajika ili kuwa na azimio moja.

Uimarishaji wa Taasisi na Kujenga Uwezo

Hatua hii itaimarisha uwezo wa watendaji wakuu na vyombo vyote katika serikali kuu na serikali za mitaa shambamba na wadu waliohusika katika kuandaa na kutekeleza Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania. Mchakato huu unatarajiwa kurahisisha ufanisi kwa kuweka miundombinu na mifumo muhimu, wafanyakazi katika ngazi ya taifa pamoja na kuweka mbinu endelevu za kupata fedha za kutekeleza mchakato mzima wa MKURABITA na urasimishaji kwa ujumla.
 

Majalida yanayohusiana
Hakuna majalida kwa wakati huu.

© Hakimiliki 2018  MKURABITA. Haki Zote Zimehifadhiwa.