Awamu ya Uandaaji wa Maboresho – MKURABITA finme кредит онлайн деньги в кредит киев срочный займ онлайн на карту украина онлайн кредит под 0

inapakia

Awamu ya Uandaaji wa Maboresho

Awamu hii ilianza kutekelezwa Janauri, 2006 na kukamilika Mei, 2008. Awamu hii ilijikita katika kuweka misingi imara ya kiutawala ya kurasimisha rasilimali na biashara inayoendana na sheria zilizopo na mifmu ya kijamii na umiliki mali na biashara kama ilivyobainishwa katika tathmini. Awamu hii ililenga ktuoa mapendekezo ya maboresho ya kisera, kisheria na kitaasisi, pamoja na mbinu za utekelezaji wa maboresho na mkakati wa kurasimisha rasilimali na biashara zilizokatika sekta isiyo rasmi kuingia katika sekta rasmi ili kuchangia ukuaji wa uchumi, kuongeza pato la taifa kwa kupanua wigo wa kodi na hatimaye kupunguza umaskini.

Uandaaji wa maboresho kwa lengo la kuondoa vikwazo vilivyobainishwa katika tathmini ya sekta isiyo rasmi ulizingatia maeneo makuu yafuatayo

 1. Kuhakiki taarifa za uchambuzi wa mifumo ya kijamii isiyo rasmi kama ilivyobainishwa katika tathmini ya awamu ya kwanza
 2. Kufanya tathmini ya kuandaa mfumo mpya utakaojumuisha mifumo isiyo rasmi ya kumiliki na kufanya biashara katika sekta isiyo rasmi na mifumo rasmi ya kisheria na kitaasisi:
 3. Kujifunza kupitia maboresho na mipango inayoendelea:
 4. Kujifunza kutokana na miradi ya majaribio inayoendelea; na
 5.   Kuoanisha mipango ya maboresho, sera na mikakati mingine ya kitaifa.

Shughuli kuu zilizotekelezwa katika awamu ya pili ni pamoja na;

 • Kuangalia upya mifumo ya sheria za rasilimali na biashara kwa kuzingatia matokeo ya utafiti
 • Kuandaa mapendekezo ya kuundwa kisheria kwa chombo kitakachoshughulikia mchakato wa kurasimisha rasilimali na bishara (chombo hiki kitatabulika kisheria na kitapewa jukumu la kutekeleza na kusimamia shughuli za mchakato wa urasimishaji rasilimali na biashara)
 • Kuandaa mpango mkakati wa utekelezaji unaoainisha kazi zilizopangwa kufanyika, muda wa utekelezaji na bajeti.
 • Kupendekeza na kuafikiana juu ya ufadhili wa kifedha kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango
 •   Kuandaa na kutekeleza mkakati wa mawasiliano ambao utaunganisha kikamilifu MKURABITA na mikakati ya kitaifa na sekta mbalimbali

Matokeo ya Maboresho ya Rasilimali na Biashara
Matokeo ya Awamu ya Pili yanajumuisha maeneo makuu matano ya mapendekezo ya maboresho ambayo utekelezaji wake utawawezesha wamiliki rasilimali kutambulika kisheria na kutumia rasilimali hizo kujinufaisha kiuchumi kwenye mifumo ya uchumi wa soko. Matokeo mengine yaliyopatikana katika awamu ya pili ni pamoja na uandaaji wa Mkakati wa Mawasiliano na Mpango Kazi wake; Tathmini ya faida zinazothibitisha umuhimu wa kuwekeza katika MKURABITA; na Mpango wa ufuatiliaji na tathmini ya mchakato mzima

Maeneo Makuu ya Maboresho
Maeneo makuu matano yamependekezwa ili kutoa mfumo bora wa sera, sheria pamoja na mfumo wa kitaasisi katika kutekeleza Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania. Maeneo haya ni pamoja na;

 • Maboresho yatakayowezesha urasimishaji wa rasilimali na biashara nchini kwa haraka na gharama nafuu
 • Maboresho yatakayowezesha matumizi ya mchakato wa kuziunganisha rasilimali zisizo rasmi na matumizi ya kiuchumi kuwa wa haraka na gharama nafuu
 • Maboresho yatakayowezesha urasimishaji wa biashara kuwa wa kasi na gharama nafuu Tanzania
 • Maboresho yatakayowezesha urasimishaji wa biashara kuwa wa kasi na gharama nafuu Tanzania.
 • Maboresho yatakayowezesh kukua kwa biashara na kutumia mali za biashara kiuchumi.
 •   Maboresho yatakayolenga masuala mtambuka kama vile, vitambulisho vya watu binafsi, kurahisishwa kwa masuala ya kiutawala, kuundwa kwa Taasisi itakayoshughulikia urasimishaji wa rasilimali na biashara.
Majalida yanayohusiana
Hakuna majalida kwa wakati huu.

© Hakimiliki 2018  MKURABITA. Haki Zote Zimehifadhiwa.