inapakia

Awamu ya Kuimarika kwa Mitaji na Utawala Bora

Awamu hii itatekelezwa sambamba na Awamu ya Utekelezaji na itaitajika katika maeneo makuu mawili ambayo ni, Kuimarika kwa Mitaji na Utawala Bora. Shughli ziatakazotekelezwa katika awmau hii zitajumuisha mchakato mzima wa kuweka na kutekeleza mapendekezo yatakayoziunganisha rasilimali zilizorasimishwa na masoko rasmi katika ngazi ya taifa na kimataifa ili kuwezesha mali zilizorasimishwa ktumika kwa Dhamana kwa lengo la kuongeza mitaji na pato.

Mchakato huu pia utahusisha uandaaji wa taratibu za mikopo, Dhamana, viwango vya riba na mfumo wa ukusanyaji kodi na madeni. Pia utajumuisha utaoaji wa huduma za Nyumba na miundomboinu, upatikanaji wa bima na mifumo ya utambulisho na utumiaji wa rasilimali kuongeza uwajibikaji.

Mapendekezo yatakayotolewa yatawezesha kuboresha utawala bora kwa kutoa taarifa za uhakika juu ya mienendo ya masoko, rasilimali, na hali ya utawala wa sheria na yale yote ambayo ni muhimu katiak maendeleo endelevu.

Urahisishaji wa Taratibu za Kiutawala

Urahisishaji wa taratibu za kiutawala utatekelezwa kwa kuweka mifumo itakayotoa mdaraka mikoani na wilayani ili kupunguza mlolongo mrefu na urasimu katika masualal ya urasimishaji rasilimali na biashara. Hatua hii ni muhimu kwani itaboresha utunzaji wa kumbukumbu katika ngazi za serikali za mitaa hivyo kujenga na kuimarisha utamaduni wa uwazi na uwajibikaji kwa njia rasmi za mawasiliano.

Uhusiano Kati ya Urasimishaji na Uwezeshaji wa Wanyonge Kisheria

Dhana ya uwezeshaji wa wanyonge au maskini inalenga kuchunguza namna gani nchi mbalimbali zinaweza kupunguza umaskini kwa kufanya maboresho yanayopanua wigo na mahitaji ya kisheria ili watu wengi waweze kunufaika na fursa nyingi za kiuchumi. Ajenga ya kuwawezesha wanyonge kisheria imejengwa katika misingi/mihimili mikuu minne nayo ni upatikanaji wa haki na utawala wa sheria, haki ya kumiliki mali, haki za kazi, na haki za kumiliki na kufanya biashara.

Jukumu la MKURABITA linahusiana moja kwa moja na mhimili wa pili na wa nne katika Ajenda hii. Ingawa inaonekana kutakuwa na uhusiano usio wa moja kwa moja na mhimili wa kwanza na wa tatu, utekelezaji wa mpango kazi wa MKURABITA na mipango mingine inayoendelea vitaendelea kuweka jitihada za kutekeleza mhimili hii. Pamja na hayo, ni muhimu kusisitiza ukweli kuwa hatima ya MKURABITA ni kuzitafsiri haki za kumiliki rasilimali na biashara kuwa manufaa ambayo walengwa wanaweza kuyaona moja kwa moja. Kwa maana hiyo, Mpango huu utatumia dhana na umuhimu wa uwezeshaji kisheria na kuweka mipango ianyotumia rasilimali na biashara hizo.

Kubaini Wadau na Kutekeleza Mfumo wa Ushirikishwaji

Kubaini wadau, kuweka mfumo wa ushirikishwaji na utekelezaji wake vitafanywa kwa kuhimiza uanzishwaji wa mfumo mmoja wa usajili utakaobainisha watu binafsi, anuani zao, mahali wanakotoka na maliwalizonazo. Pia itafuatilia mabadiliko muhimu ambayo yanaathiri biashara katika soko.
 

Majalida yanayohusiana
Hakuna majalida kwa wakati huu.

© Hakimiliki 2018  MKURABITA. Haki Zote Zimehifadhiwa.

blog lam dep | toc dep | giam can nhanh

|

toc ngan dep 2016 | duong da dep | 999+ kieu vay dep 2016

| toc dep 2016 | du lichdia diem an uong

xem hai

the best premium magento themes

dat ten cho con

áo sơ mi nữ

giảm cân nhanh

kiểu tóc đẹp

đặt tên hay cho con

xu hướng thời trangPhunuso.vn

shop giày nữ

giày lười nữgiày thể thao nữthời trang f5Responsive WordPress Themenha cap 4 nong thonmau biet thu deptoc dephouse beautifulgiay the thao nugiay luoi nutạp chí phụ nữhardware resourcesshop giày lườithời trang nam hàn quốcgiày hàn quốcgiày nam 2015shop giày onlineáo sơ mi hàn quốcshop thời trang nam nữdiễn đàn người tiêu dùngdiễn đàn thời tranggiày thể thao nữ hcmphụ kiện thời trang giá rẻ