September 21, 2016 Uncategorized 0 comment

MKURABITA Wajumuika Matembezi ya Hisani Kusaidia Wahanga wa Tetemeko la Ardhi Kagera

IMG-20160917-WA0001

 

MKURABITA ni moja ya taasisi zilizoko chini ya Ofisi ya Rais Ikulu ambayo iliguswa na janga lililowapata ndugu zetu wa mkoa wa Kagera kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea tarehe 10 Septemba 2016. Katika kudhihirisha kuguswa na tukio hilo, wafanyakazi wa MKURABITA waliungana na wafanyakazi wengine kutoka taasisi za umma, binafsi, mashirika ya kimataifa, mabalozi na watu wote wenye mapenzi mema katika matembezi ya hisani.

 

Matembezi haya yaliongozwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi yalianzia na kuishia Bwalo la Polisi Oysterbay mnamo tarehe 17 Septemba 2016 kwa ajili ya kuchangia wahanga wa tetemeko hilo.

 

Katika picha ni baadhi ya watumishi wa MKURABITA wakijiandaa kuanza matembezi