our newsAllahmagazine and celebrityfirst class business ideas & tipsplaces map directorycooking tipsallah ve mehdiveysel karani ve evliyalar money us samples of business plans what is a good business to start what kind of business should i start health loss
 
 
 
Karibu

Karibu kwenye tovuti ya MKURABITA- Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania Mpango ambao umeanzishwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpango huu umeanzishwa kwa lengo la kuwapa nguvu ya kiuchumi wananchi hasa wale wa kipato cha chini (wanyonge) vijijini na mijini kwa kuwaongezea uwezo wa kumiliki na kufanya biashara katika mfumo rasmi wa kisasa, unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria za kanuni rasmi za kiutawala. Hivyo kwa kupitia urasimishaji raslimali na biashara, MKURABITA ni nyezo ya uwezeshaji wa Watanzania kiuchumi.

  
 
 • HABARI
 • MATUKIO
 • SHUHUDA
 • TAARIFA

 
 
 • Hakikisha kuwa mipaka ya kijiji imehakikiwa na kupimwa ipasavyo ili kuepusha migogoro ya mipaka na vijiji jirani
 • Kijiji kiwe kimesajiliwa na kupata Cheti cha Ardhi ya Kijiji
 • Kijiji kiwe na jengo linalofaa kwa Masjala ya ardhi ya Kijiji
 • Maombi ya kupimiwa na kupata hati miliki ya kimila yapelekwe kwenye Halmashauri ya Kijiji kwa ajili ya mapendekezo ya kuidhinishwa
 • Maombi lazima yapitishwe na kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji
 
 
 • Kutambuliwa na kuainishwa kwa eneo la urasimishaji na Halmashauri husika katika mji, Manispaa au Jiji,
 • Uhamasishaji kwa Uongozi na wananchi wa eneo la urasimishaji,
 • Utayarishaji wa michoro ya mipango miji na kuidhinishwa na mamlaka husika,
 • Upimaji ardhi ya wananchi kulingana na michoro ya mipango miji
 • Uidhinishaji wa ramani za upimaji kwenye mamlaka husika,
 • Utayarishaji na utoaji wa Hati za kumiliki ardhi kwa wamiliki wa ardhi iliyopimwa.